0
CHAMA  cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini ( IGP),  Simon  Sirro kuacha kutoa vitisho kwa wananchi na wanasiasa kwa kuwataka waache kuzungumzia tukio la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  (Tundu Lissu kupigwa risasi 38 mkoani Dodoma kwa kuwa hiyo siyo kazi yake, anaandika Mwandishi wetu.
Chadema wamesema hakuna sheria yoyote inayompa Sirro mamlaka hayo na kwamba anatakiwa kuacha kutoa kauli za kuwanyamazisha.
Kauli hiyo ya Chadema, imetolewa leo na Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya  alipozungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho.
Amesema Sirro hana ubavu wa kuzuia watu wakiwamo wanasiasa kuendelea kujadili suala hilo.
“Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki na fursa kwa wananchi kutoa maoni na mawazo yao na kupashana habari pamoja na sheria nyingine na  ibara hii ndio msingi, ” amesema Malya.
CHANZO:MWANAHALISI ONLINE

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top