Diwani
wa Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha, Ahimidiwe Rico amewasilisha
kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kifaa anachodai
alikitumia kuwarekodi waliomshawishi kujiuzulu wadhifa huo.
Baada
ya Oktoba 17,2017 kuhojiwa na maofisa wa Takukuru, jana Oktoba 19,2017
Rico alifika ofisi za taasisi hiyo saa nane mchana kukabidhi kifaa hicho
chenye umbo la kalamu anachodai kimetengenezwa nchini Ujerumani.
Akizungumza
na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi kifaa hicho, alisema
ameitikia wito wa maofisa wa Takukuru waliomtaka akiwasilishe.
Alisema
anasimamia ukweli ambao utamuweka huru na haogopi kwa kuwa katika siku
za hivi karibuni amekuwa akipokea baadhi ya vitisho kutoka kwa watu
wanaomtaka asijihusishe na sakata hilo.
Diwani
huyo wa Chadema alisema tangu aanze kushawishiwa apokee rushwa kwa
lengo la kujiuzulu nafasi yake alirekodi matukio yote na mawasiliano
ambayo amekuwa akiwasiliana na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Post a Comment
karibu kwa maoni