Katika hali isiyo ya kawaida Padri wa kanisa Katoliki Babati kigango cha Managha ambacho huwa kinapata Misa kila jumapili amegoma kuongoza ibada leo.
Kisa cha kugoma kuongoza misa hiyo ni baada ya kukosa taarifa ya Zaka aliyohitaji apatiwe kutokana na mtoa taarifa kukosekana.
Taarifa inaeleza kuwa mtoa taarifa aliomba udhuru mapema kwamba hatokuwepo,amesafiri na kwaya ya kanisa kwa ajili ya kuinjilisha huko Nangwa wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Padri Nakei alisema hawezi kuendelea na misa hiyo bila kupata taarifa kuhusu Zaka.
Nikukumbushe tu kuwa Zaka ni Zaka ni asilimia kumi (10%) ya pato la mtu kwa mwaka ambalo anapaswa kulitoa kwa Kanisa.
Post a Comment
karibu kwa maoni