Jeshi la
polisi mkoani MANYARA linamshikilia mkazi wa Kijungu wilaya ya KITETO kwa kumiliki silaha aina ya
Bunduki [GOBORE] kinyume na taratibu za nchi ya Tanzania.
Mtuhumiwa
anayeshikiliwa na jeshi la polisi ni Sikujua Kalulu [32] Mgogo mkazi wa
kitongoji cha kona Kijungu aliyepekuliwa
nyumbani kwake baada ya polisi waliokuwa doria kupata taaifa kutoka kwa raia
wema na kukuta silaha hiyo chini ya
godoro.
Mtuhumiwa
huyo alipekuliwa na polisi hao majira ya saa sita mchana tarehe 26 novemba
mwaka huu huku mashuhuda wakishuhudia.
Silaha hiyo
ipo mikononi mwa jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi japo uzoefu unaonyesha kuwa silaa kama hizo hutumika
katika kufanyia ujangili na matukio mengine ya uhalifu.
Akizungumza
na mtandao huu kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga ameeleza kuwa
mtuhumiwa huyo anaendelea kuchunguzwa na muda wowote atapandishwa kizimbani.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga
amewataka wakazi wa Manyara kutoa ushirikiano katika jeshi hilo ili kukomesha
vitendo vya uhalifu.
Hata hivyo
kwa sasa jeshi hilo mkoani Manyara limeendelea na doria mbalimbali mchna na
usiku ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na watu wasio na mapenzi
mema na nchi yao.
Kwa upande
mwingine Kamanda Senga amesema kuwa katika kuelekea katika siku kuu za mwisho
wa mwaka jeshi la polisi mkoani Manyara limejidhatiti vyema katika kupambana na
vitendo vyote vya uhalifu huku akiwataka wananchi kuripoti katika kituo cha
polisi pindi wanapoona vitendo vya uvunjifu wa
amani.
Post a Comment
karibu kwa maoni