0

Baba wa familia ya watoto wa tatu aliyetambulika kwa jina la Magnus Nsikak, miaka 40 na mkewe Ruth Nsikak wamekamatwa kwa kosa la kuwauza watoto wao akiwemo binti yao wa miaka 10 aitwaye Ekpo, Ubong mika 5  na kichanga cha siku tatu.Polisi mjini Akwa Ibom, Nigeria wamewakamata wanandoa hao waliouza watoto wao watatu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Dail Mail unaeleza kuwa wazazi hao walikamatwa baada ya kuwekewa mtego na Wauguzi wa Hospitali ya Serikali ya Ikot-Abaji katika jimbo la Abia.
Mwanamke huyo, Ruth amesema mapema baada ya kujifungua jumatatu ya wiki iliyopita mme wake alimwambia kuwa mtoto wao amefariki hivyo alimuamuru warudi nyumbani.
Akitoa maelezo polisi mmoja wa Wauguzia katika Hospitali hiyo amesema Mwanaume huyo alimurubuni kumpa pesa ili amuachie kichanga huyo lakini alikaa na baadae usiku mwanaume huyo alitoroka na kichanga hicho.
Kwa upande mwingine Ruth amekataa kuhusika na kuuza watoto wake akidai baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki alirudi nyumbani kuendelea kujiuguza huku akikiri wazi kuwa aliletewa kiasi cha Naira 20,000 sawa na tsh 125,000/=.
Hata hivyo kwenye mahojiano hayo mwanamke huyo aliulizwa idadi ya watoto waliozaa na mwanaume huyo ndipo sakata lingine likaibuka baada ya kusema kujibu kuwa wamezaa watoto watatu lakini wote wapo kwa ndugu wa Mwanaume.
Ndipo mwanaume alipoambiwa apige simu kwa ndugu zake wajue kama watoto hao wako salama au laah! jambo ambalo mwanaume alikataa kutoa ushirikiano na polisi.
Mwanamke alionesha ushirikiano na polisi kwa kuwapa namba za simu za mama yake mzazi na Maguus anayeishi mjini Lagos, ambapo baada ya kupigiwa simu alisema ana muda mrefu hajawahi kuwaona wajukuu wake.
Polisi walichukua uamuzi wa kumbana mtuhumiwa ndipo alipoweka wazi kuwa alimdanganya mkewe kuwa watoto wao wawili aliwapeleka kwa ndugu zake lakini kumbe haikuwa hivyo bali aliwauza kwa kiasi cha Naira 150,000/= sawa na tsh milioni 10 ili kupunguza matatizo ya kifamilia ikiwemo kodi ya nyumba.
Kamanda wa Polisi mjini Akwa Ibom, Kamanda Zubairu Muazu amesema bado wanawashikiria wazazi hao kwa uchunguzi zaidi kabla ya kuwapeleka mahakamani kujibu tuhuma hizo za uuzaji wa watoto.
Tulifanikiwa kuongea na wazazi wote kwa undani zaidi na Mwanaume amekiri kufanya uovu huo. Tumepata mahojiano pia na kaka wa Mwanamke ambaye Magnus awali alisema watoto wake aliwapeleka huko lakini kumbe hajawahi kuwaona miaka miwili sasa. Upelelezi bado unaendelea na watuhumiwa wapo chini ya polisi hadi upelelezi utakapokamilika.amesema Kamanda Zubairu kwenye taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Sun.
Kwa mujibu wa maelezo Hilo linakuwa ni tukio la nne kwa mwaka huu nchini Nigeria baada ya mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Eucharia Daniel kutoka mjini Akwa Ibom kukamatwa na polisi mwezi septemba kwa kujihusisha na ununuzi wa vichanga nchini humo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top