Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi akitoa ufafanuzi na kutoa maagizo ya serikali katika baraza la madiwani Hlamashauri ya wilaya ya Babati leo novemba 1. 2017. |
Madiwani hao wameeleza kuwa kikosi hicho kimekuwa kikifanya tofauti na kusudio lililopangwa kwani wanatumia nguvu kubwa kwa kuwapiga watu wakiwemo viongozi bila kufuata taratibu.
Madiwani hao wamesema Kuwa polisi hao wamekuwa wakifika katika maeneo mbalimbali na kuwakamata na kuwaumiza watu kinyume cha sheria.
Madiwani hao wameongeza kuwa hawapingi jeshi la polisi kuanzisha kikosi hicho kwa ajili ya kupambana na uhalifu na madawa ya kulevya ndani ya mkoa wa Manyara lakini wamekuwa wakikiuka wanapofika vijijini na maeneo mengine.
Kama wangekuwa wanafanya kazi waliotumwa basi mkoa wetu usingekuwa na pombe za moshi wala wavuta bangi na wauza bangi' waliongeza madiwani hao kwa msisitizo.Mkuu wa wilaya ya Babati Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Raymond Mushi amesema hilo ameliwasilisha kwa uongozi Wa juu wa Jeshi la polisi mkoa wa Manyara na kuahidi kuitisha kikao Maalum kati ya RPC na madiwani muda wowote.
Ikumbukwe Kuwa sio mara ya kwanza kulalamikiwa,hata madiwani Babati mjini walishawalalamikia polisi hao.
Post a Comment
karibu kwa maoni