Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati Mohamedi Kibiki akishuhudia michuano ya Kololi Cup,kulia ni mdhamini wa michuano hiyo Abrahamani Kololi. |
Katika michuano hiyo iliyokusanya kijiji cha Malangi rika zote na jinsia zote baadhi ya michezo ilichezwa hali ya kuwa mvua inanyesha.
Hiki ni kikosi cha timu ya Young Nation kutoka Kiongozi |
Kibiki amesema ameguswa na michuano hiyo na kuahidi kuanzisha ligi kama hiyo katika kata yake ya Babati mjini japo hakusema itaanza lini.
Kwa upande wa mdhamini wa ligi hiyo Abrahamani Kololi amesema kuwa michuano hiyo itafanyika kila mwaka na bado ataendelea kuipa nguvu KOLOLI CUP kwa kutoa zawadi nono zaidi ya hizo alizozitoa kwa timu zinazoshinda na mchezaji bora.
Mchezo wa mwisho wa kumtafuta mshindi wa tatu ulipigwa kati ya Ruby Star ya Malangi dhidi ya Young Nation ya kiongozi mchezo ambao umeshuhudia Ruby Star ikishinda na kuchukua dume la Ng'ombe baada ya kupata ushindi wa 1-0 walilopata kwa kuwachapa Young Nation.
Mshindi wa pili alichukua Sinai Rangers iliyokabidhiwa mbuzi dume [beberu] mshindi wa tatu ambaye ni Dogo dogo Fc alikabidhiwa shilingi elfu hamsini taslimu 50,000.
Beberu waliozawadiwa washindi wa pili Sinai Rangers. |
Ikumbukwe kuwa michuano hiyo ilianza mwezi novemba 4 2017 kwa kuzikutanisha timu tano ambazo zote zinatoka katika kata ya Maisaka ambazo Sinai Rangers,Ruby Stars,Dogo dogo Fc na Sawe Fc.
Kikosi cha wachezaji timu ya Ruby Stars kutoka Malangi. |
WALTER HABARI, kuanzia hatua ya kwanza ya michuano hiyo ilikuwa ikifuatilia huku ikiruka hewani kupitia vipindi vya michezo M fm ,hongera sana diwani Kololi ka kuthamini Michezo hivyo na wengine katika kata zao waige mfano huo.
Post a Comment
karibu kwa maoni