0


Mwandaaji wa Ligi ya KOLOLI CUP diwani wa kata ya Maisaka mjini Babati mkoani Manyara mheshimiwa Abrahamani Kololi akishuhudia mchezo kati ya Sinai Rangers vs Sawe Fc.
Mashabiki.

Ligi ya diwani wa Maisaka Abahamani kololi imeendelea tena leo katika uwanja wa shule ya msingi Malangi mjini Babati mkoani Manyara kwa kuwakutanisha miamba ya Soka Babati Sinai Rangers dhidi ya Sawe Fc mpira ukichezwa wakati mvua ikiendelea kunyesha.
Katika mchezo huo Sinai Rangers Imeibuka kwa ushindi wa mabao 4-2 Sawe Fc,na kwa maana hiyo Sinai Rangers imefikisha pointi 6,mabao 9, na kuapanda juu katika ligi hiyo inayotarajiwa kukamilika novemba 13.
Ruby Star kutoka Malangi ina point 4 mabao 3,Young Nation ina pointi 3,mabao 3.
Mchezaji wa timu ya Sinai Rangers Kenneth Makotha aliefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Sawe Fc anaeonekana upande wa kulia akiwa na tabasamu wakati wa mapumziko.
WALTER BLOG imezungumza na viongozi wa Sinai Rangers na Sawe Fc  ambao wameeleza kuwa ligi ni ngumu ila wote wanaoyo matumaini ya kushinda.
Walimu wa timu ya Sinai Rangers Silas Michael kushoto na Msaidizi wake Juma Swalehe kulia wakiweka sawa jambo.
Mwalimu wa Sawe Fc  Imma Tango ametupia lawama waamuzi wasaidizi kwa kushindwa kutoa maamuzi sahihi kwa mchezaji,”wengine wachezaji wa timu pinzani wanapiga wenzao uwanjani lakini hakuna maamuzi yanayochukuliwa,maamuzi sio mazuri”,alisisitiza Tango.
Kocha wa Sawe Fc Imma Tango akiwashuhudia vijana wake uwanjani.
Kwa upande wa Kocha wa timu ya Sinai Rangers Silas Michael [KIROHO SAFI] akizungumzia waamuzi katika mchezo huo alisema waandaaji ligi kama hizo wanapoanzisah wahakikishe waamuzi wote wanaopatikana wanaelewa mpira na kutoa maamuzi amabayo hayatapendelea upande wowote ili kuepusha lawama na fujo uwanjani.
Mwonekano wa koha wa Sinai Rangers Silas Michael [Kiroho Safi] baada ya kufungwa bao la pili na Sawe Fc.
Mwandaaji wa ligi hiyo ya Kololi Cup Diwani wa kata ya Maisaka Abrahaman Kololi amezitaja zawadi watakazopatiwa washindi,mshindi wa kwanza atapata dume kubwa la Ng’ombe,mshindi wa pili Beberu huku mshindi wa tatu akipatiwa shilingi 50,000 za kitanzania.
Timu zikiwa uwanjani Kumenyana
Kololi amesema mashindano haya yatafanyika kila mwaka katika muda wote atakaokuwepo madarakani.
Wakina dada wakishuhudia mechi.
Ligi hii yenye mamia ya mashabiki inashuhudiwa pia na wakina mama na kina dada ambao imekuwa ni mara chache sana kuonekana viwanjani kuangalia mchezo huo wa mpira wa Miguu.
Mashabiki wakishuhudia mchezo katika uwanja wa shule ya Msingi Malangi.
Kololi Cup 2017 inatarajiwa kukamilika novemba 13 mwaka huu ikifungwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Mohammed Kibiki ambaye pia ni diwani wa kata ya Babati mjini.
Timu zinazoshiriki zote zinatokea katika kata ya Maisaka,timu hizo ni Rubi Star,Sawe Fc,Sinai Rangers,Dogodogo Fc na Young Nation.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top