Wanafunzi wanaohitimu katika vyuo mbalimbali vya
ufundi Stadi hapa nchini wametakiwa kutumia mafunzo wanayopatiwa katika
kujiajiri.
Wito huo umetolewa na mkuu wa mafunzo Wilbert
Bendera katika mahafali ya nne kwa
wanafunzi wa mwaka wa pili 168 wanaohitimu katika chuo cha Ufundi stadi Manyara
[VETA] katika fani tisa.
Bwana Bendera amewataka wazazi na walezi
wanaowasiamia wanafunzi hao waliohitimu kuwasaidia kupata nyenzo
zitakazowafungulia njia kuweza kujiajiri.
Ernest Msumari na Betsheba John ni wahitimu
wanaeleza kuwa baada ya kupata maarifa na ujuzi mbalimbali waliopatiwa wakiwa
chuoni wataweza kujiajiri na kujitegemea.
Katika kuendeleza kilimo mkoa wa Manyara chuo
hicho pia kimeandaa kozi maalumu itakayoaanza mwaka ujao..
Kwa mwakani tutakuwa na mfumo mpa wa kufundisha DUO kwa ufadhili kutoka nchi ya Ujerumani kujifunza shuleni na eneo la kazi kulingana masomo ya mhusika.
Chuo cha VETA MANYARA ni miongoni mwa vyuo 28
vinavyomilikiwa na mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi [VETA]
kilianzishwa mwezi wa kwanza mwaka 2012 na kuzinduliwa rasmi mwezi wa nne mwaka
2012.
Courses zinazotolewa na sifa za kujiunga
ReplyDelete