Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imepitia ripoti za michezo yote ya Ligi Kuu Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja Pili (SDL) na kufanya uamuzi ufuatao.
Mechi namba 16 Kundi A (Friends Rangers 1 v African Lyon 1). Klabu ya African Lyon imepewa Onyo Kali kwa timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 20 Kundi A (Mgambo JKT 1 v Mshikamano 0). Klabu ya Mgambo JKT imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo kupulizwa. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 21 Kundi A (Kiluvya United 2 0 v Mshikamano 1). Klabu ya Kiluvya United imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Faini hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 24 Kundi A (Friends Rangers 0 v JKT Ruvu 3). Klabu ya Friends Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kusababisha mchezo kusimama kwa dakika tano baada ya kumpiga jiwe Mwamuzi Msaidizi. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 28 Kundi A (Mgambo JKT 2 v Ashanti United 1). Klabu ya Mgambo JKT imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 13. Adhabu hiyo ni utekelezaji wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 15 Kundi B (KMC 1 v Mbeya Kwanza 0). Mchezaji Stephano Mwasika wa KMC amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kumpiga kiwiko kwa makusudi mchezaji wa Mbeya Kwanza. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Mechi namba 17 Kundi B (JKT Mlale 1 v Polisi Dar 1). Klabu ya JKT Mlale imepewa Onyo Kali kwa timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Klabu ya Polisi Dar imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 15. Adhabu hiyo ni utekelezaji wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 19 Kundi B (Coastal Union 1 v Polisi Tanzania 1). Wachezaji Athuman Idd Chuji wa Coastal Union na Shabani Stambuli wa Polisi Tanzania wamesimamishwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kila mmoja kwa kosa la kupigana uwanjani. Adhabu dhidi yao ni kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Mechi namba 21 Kundi B (Mbeya Kwanza 0 v JKT Mlale 0). Klabu ya JKT Mlale imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 23 Kundi B (Mawenzi Market 0 v Mufindi United 1). Klabu ya Mawenzi Market imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kusababisha mchezo kusimama kwa dakika nne baada ya kumpiga jiwe Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 13 Kundi C (JKT Oljoro 1 v Toto Africans 0). Klabu ya Toto Africans imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 17 Kundi C (Dodoma FC 1 v JKT Oljoro 0). Mwamuzi Said Pambalelo amepewa Onyo Kali kwa kutochukua hatua dhidi ya wachezaji wa JKT Oljoro waliokuwa wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume na kanuni za mpira wa miguu. Adhabu dhidi yake ni kwa mjuibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Mechi namba 26 Kundi C (Transit Camp 1 v Biashara United Mara 0). Klabu za Transit Camp na Biashara United Mara kila moja imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na timu zao kuonesha vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina katika mechi hiyo wakati zikiingiz uwanjani. Adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Klabu ya Transit Camp pia imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo kupulizwa kwa lengo la kutaka kumpiga Mwamuzi. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 27 Kundi C (Pamba SC 1 v Rhino Rangers 0). Klabu ya Pamba imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Nayo klabu ya Rhino Rangers imepewa Onyo Kali kutokana na washabiki wa timu yake kutoa lugha za matusi wakati mchezo huo ukiendelea.
Post a Comment
karibu kwa maoni