0
Mwanaridha Ismail Juma aliefariki alhamisi kwa ajali akiwa anaendesha piki piki katika mtaa wa Nangara mjini Babati mkoani Manyara amezikwa leo na mamia ya watu nyumbani kwao kijiji cha Gendi kata ya Singe wilyani hapa.
Ismail amefariki ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu asajiliwe na kamati ya olimpiki duniani kushiriki mashindano ya kimataifa hapo mwakani.
Katibu mkuu wa riadha Tanzania Wilhelm Gidabuday akitoa salamu kutoka vyama mbalimbali vya michezo na viongozi mbali mbali,wizara ya habari na michezo na salamu kutoka kwa rais wa Chama cha riadha Tanzania ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, amesema chama na taifa limepoteza mtu ambaye rekodi yake haijafikiwa na mtu yeyote duniani mpaka sasa.
Naye mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi alihudhuria katika safari ya mwisho ya Ismail Juma na kuwataka vijana kutumia vizuri vipaji walivyonavyo wakiiga mfano wa Ismail.
Ismail alizaliwa mwaka 1991 katika kijiji cha Gidas Wilayani Babati mkoani Manyara na alianza riadha tangu akiwa mtoto,hajaacha mke wala mtoto.
Bwana ametoa,bwana ametwaa jina la Mungu lihimidiwe.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top