0
 Lazaro NyalanduSIKU chache baada ya Lazaro Nyalandu kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini, Tume ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa haina taarifa kuhusu mbunge huyo na kwamba watakapoipata watatoa utaratibu unaopaswa kuchukuliwa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima alisema hayo jana mchana, ikiwa ni siku moja baada ya Ofisi ya Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa taarifa kuwa wameshawasilisha barua kwa mkurugenzi huyo kumtaarifu shauri la Nyalandu la kupoteza sifa za kuwa mbunge.
Kailima alisema, “Mpaka sasa hatujapata taarifa yoyote kuhusu mheshimiwa Nyalandu, kama taarifa hiyo itafika kwetu tutatoa taarifa kwa umma”. Akitoa ufafanuzi kuhusu sheria zinazopaswa kufuata, alisema kuwa Ubunge unaweza kukwama pale mbunge au mbunge wa viti maalumu atakapovuliwa uanachama na chama cha siasa, au kuamua kuachana na chama.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top