0
Image result for UHURU KENYATTA KUAPISHWARais Kenyatta na Naibu Rais William Ruto wamekamilisha sherehe za leo uwanja wa Kasarani kwa maombi, Bw Kenyatta ameongoza kwa Kiingereza na Bw Ruto kwa Kiswahili.
Baadaye, wimbo wa Jumuiya ya EAC umechezwa na kisha wimbo wa taifa la Kenya kuhitimisha sherehe za leo.
Wageni wameanza kuondoka uwanjani, wakianza na viongozi wa nchi.
Kwa mara nyingine, Bw Kenyatta amewahimiza Wakenya kuishi kama majirani. Amesema majirani hufaana sana na ndio hutegemewa wakati wa shida.
Ameagiza watahiniwa wote wa darasa la nane waliofanya mtihani wao mwaka huu wawe wamefahamu shule za sekondari watakazojiunga nazo kabla ya Krismasi.
Rais Kenyatta ametangaza kwamba Mwafrika yeyote atapewa viza akifika katika kiingilio chochote mpakani au viwanja vya ndege Kenya.
Amesema hataweka masharti kwamba lazima mataifa mengine yafanye hivyo.
Amechukua hatua sawa na iliyochukuliwa na Rwanda majuzi.
Nchini Rwanda hata hivyo, ni raia wa taifa lolote lile.
Ameahidi pia kufufua moyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Amesema wananchi wa nchi wanachama watahesabiwa kama Wakenya. Watahitajika tu kutumia kitambulisho. Wanaweza kuingia au kutoka na kufanya kazi, kumiliki mali au hata kuoana bila kuwekewa masharti.
Amesema hata hivyo kwamba sheria nayo itatumika kwa njia sawa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top