Maandamano
ya aina yoyote ni haki ya mwananchi na yanaruhusiwa kisheria lakini
maandamano hayo lazima yafuate sheria na taratibu zilizobainishwa katika
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sheria
ya maandamano inamtaka mwananchi au kundi la wananchi wanaohitaji
kufanya maandamano kutoa taarifa kwa maandishi kwa Mkuu wa Polisi wa
eneo husika kabla ya masaa 48 ya kuanza kwa maandamano hayo ikieleza
dhumuni la maandamano hayo.
Pia
wahusika wanatakiwa wawe tayari kwa jibu lolote kutoka kwa mkuu huyo
kwa kuwa chochote watakachojibiwa lazima kiwe na sababu.
Endapo
wahusika watakataliwa kufanya maandamano na hawatoridhishwa na sababu
zilizotolewa na Mkuu wa Polisi kuna hatua mbili muhimu zinazotakiwa
kufuatwa na sio wahusika kujiamulia kuandamana kilazima kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.
Hatua
hizo muhimu zinazotakiwa kufuatwa ni kuandika barua kwa Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi na kumueleza kutoridhishwa na sababu zilizotolewa na
Mkuu wa Polisi ili Waziri naye kwa upande wake aamue kuruhusu au
kukataza.
Endapo
wahusika hawatoridhika na majibu ya Waziri, waandamanaji watatakiwa
kwenda Mahakamani ambapo ndipo uamuzi wa mwisho utatolewa.
Hakuna
sheria inayotambua maandamano ya nchi nzima kufanyika kwa siku moja kwa
sababu kila eneo lina Mkuu wa Polisi mwenye haki ya kukubali au kukataa
ombi la kufanya maandamano kulingana na hali halisi ya eneo lake.
Kila
jambo lina faida na hasara zake lakini kuna mambo ambayo faida huwa
chache kuliko hasara, maandamano yana athari kubwa kiuchumi na kijamii
kwa sababu maandamano yoyote ni lazima Jeshi la Polisi liwajibike katika
kuongoza na kulinda maandamano hayo, hivyo kupelekea wanajeshi wengi
kusitisha kazi zingine kwa ajili ya kuzuia vurugu zisitokee.
Athari
zingine ni kusitishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za usafiri ,
kufungwa kwa maduka na masoko pamoja na athari zitokanazo na vurugu
zinazoweza kutokea kwa sababu ya maandamano hayo.
Hivyo
itambulike kisheria hatua hizo zinatakiwa kufuatwa kabla ya kufanya
maandamano, aidha maandamano kisheria ni jambo halali endapo tu litakuwa
limehalalishwa kisheria.
Post a Comment
karibu kwa maoni