Serikali
inatarajia kununua kondomu milioni 500 zitakazosambazwa nchi nzima bure
kwa lengo la kupunguza maambukizi ya Ukimwi ifikapo mwaka 2030.
Kondomu
hizo zitasambazwa bila malipo ambapo kutakuwa na mashine maalumu
zitakazofungwa kwenye maeneo ya baa, nyumba za kulala wageni, migodini
na katika kumbi za burudani.
Akizungumza
leo wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kondomu, Mkurugenzi wa
Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk. Neema Rusibamaila, amesema kondomu hizo zitanunuliwa kupitia
fedha za Global Fund.
“Takwimu
za mwaka 2011/12 zinaonyesha asilimia 69 ya wanawake na asilimia 77 ya
wanaume wanafahamu kwamba kondomu inaweza kuzuia VVU lakini ni asilimia
27 tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja walitumia kondomu walipofanya
ngono mara ya mwisho,” amesema.
Post a Comment
karibu kwa maoni