0
Image result for STAND YA MABASIMamlaka ya udhibiti na usafiri wa nchi kavu na majini [SUMATRA] imewataka wamiliki na madereva pamoja na  makondakta  wa magari kutekeleza agizo la nauli zilizopangwa na mamlaka hiyo.
Akizungumza na kituo hiki afisa mfawidhi wa SUMATRA mkoa wa Manyara Nelson Mmary amezitaja bei anazopaswa kulipia abiria,Kwa Babati-Singida nauli ni shilingi 5,900,Babati-Dodoma shilingi 13,800,Babati -Arusha shilingi 6,000,Babati-Katesh shilingi 2600.
Pia Sumatra imewakumbusha  madereva na makondakta kuvaa sare za kazi pindi wanapokuwa katika majukumu yao.
 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top