Wakulima wa mbaazi mjini Babati mkoani Manyara wameiomba
serikali kuwahakikishia soko la zao hilo kwa msimu wa mwaka 2018 ili waamue
kulima zao hilo ama kuacha baada ya soko la mbaazi kuporomoka mwaka huu wa 2017
na hali ya maisha yao kuwa magumu
Sambamba na hilo wakulima hao wameiomba serikali kuwatafutia ufumbuzi wa changamoto ya
upatikanaji wa soko la uhakika
Wakizungumza kwa masikitiko kuhusiana na hali hiyo
wafanyabiashara Rukia Chikawa na
Josephat Dickson wameeleza zao la
mbaazi ndio zao ambalo walikuwa wakilitegemea kwa ajili ya biashara na kuweza
kuwapatia mbegu za mazao mengine pamoja na pembejo nyingine za kilimo
Aidha kwa upande wa serikali ya awamu ya tani imekuwa
ikisisitiza kuwa inamjali mnyonge na
kuhakikisha haki ya mnyonge inapatikana katika kutatua changamoto mbalimbali,
hivyo mkulima wa chini anaitegemea serikali katika kumtafutia urahisi wa kuapata masoko.
Post a Comment
karibu kwa maoni