Anaandika Suleiman Ussi kutoka Zanzibar
Kikosi cha timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kinaendelea na mazoezi yake kujiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017 huko nchini Kenya.
Mazoezi hayo
yanayosimamiwa na kocha mkuu wa kikosi hicho Hemed Suleiman (Morocco)
yanaendelea kila siku kuanzia saa 2:00 za asubuhi katika uwanja wa Amaan Mjini
Unguja.
Mpaka sasa wachezaji
waliyoanza mazoezi ni wale ambao vilabu vyao vya Unguja huku ikiwa bado makundi
mawili kutoka Kisiwani Pemba na Tanzania Bara bado hawajajumuika na wenzao
ambapo wale kutoka Pemba wakitarajiwa kesho kuungana na wenzao.
Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed Ali
"Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman
"Wawesha" (JKU), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm
Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz"
(Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya
Jang'ombe).
Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul
Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad
Mshamata (Chuoni) pamoja na washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais"
(Jang'ombe boys) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).
Ambao bado hawajawasili kutoka Pemba ni Mlinda mlango
Nassor Mrisho (Okapi), Viungo Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi) na
Mbarouk Marshed (Super Falcon) pamoja na mshambuliaji Mwalimu Mohd (Jamhuri).
Wachezaji ambao wanatokea ligi kuu soka Tanzania bara
ambao bado hawajajumuika na wenzao ni Walinzi Abdallah Haji "Ninja"
(Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali
(Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir Yahya (Singida
United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar) na Suleiman Kassim
"Seleembe" (Majimaji) pamoja na washambuliaji Kassim Suleiman
(Prisons), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli).
Post a Comment
karibu kwa maoni