0


Mtu mmoja  mkazi wa mtaa wa Arri Nangara mjini Babati  mkoani Manyara, Kidess Mgala mwenye umri kati ya miaka 30- na 35 amefariki dunia baada ya kujinyonga.
Tukio hilo limetokea ijumaa 29.12.2012  majira ya saa tatu asubuhi katika mtaa wa Arri kata ya Nangara mjini Babati.
Mwenyekiti wa mtaa huo Nicholaus Sebastian Kilongo alithibitisha mtu huyo kujinyonga huku akisema ni tukio lililowahuzunisha wengi kwani kijana huyo hakuwahi kuwa na ugomvi na mtu yeyote kijijini hapo.
Mtu  huyo alitumia kamba ya katani kujinyonga akiifunga kwenye mti .
Kamanda wa polisi mkoani hapa Agustino Senga amesema marehemu alikutwa na ujumbe katika mfuko wa suruali yake aliyokuwa ameivaa uliosomeka kuwa ‘nimeamua kujinyonga kutokana na ugomvi wa kifamilia’ japo hakusema ni ugomvi wa aina gani.
Senga ameendelea kutoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi na kuwashauri kutoa taarifa kwa ndugu au rafiki endapo kutakuwa na jambo na sio kuchukua maamuzi ya kujiua.
Wakazi wa mtaa huo walijitokeza kwa wingi kushuhudia mwili wa marehemu ukiwa unaning’inia huku ndugu zake wa karibu wakielezea tukio hilo kwa majonzi makubwa.
Hata hivyo marehemu amekutwa na ujumbe mfukoni ambao kwa haraka hatujaweza kujua nini kimeandikwa katika karatasi hiyo.
Mwili wa marehem umechukuliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kidaktari na umehifadhiwa katika chumba cha kuhidhia maiti katika hospitali ya mji wa Babati Mrara.
Hata hivyo kamanda Senga wiki hii akizungumza na waandishi wa habari aliwahakikishia wakazi wa mkoa wa Manyara kuwa msimu wa siku kuu za mwisho wa mwaka ulinzi na usalama utaimarishwa kila kona na kuwataka watoe ushirikiano kwa jeshi hilo pindi wanapobaini  uhalifu vitendo vya uvunjifu wa amani.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top