0



Mtu  mmoja aliyefahamika kwa majina ya Hussein Ndume mkazi wa kijiji cha Galapo wailaya ya Babati mkoani Manyara  amenusurika kifo baaada ya kukatwa vidole vitatu vya mkono wake walipokuwa katika ugomvi usiku wa Chrismass.
Tukio hilo limetokea majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo karibu na Grocery iitwayo Metalic Pub amabapo wawili hao wakiwa tayari wamelewa walianza kuzozana ndipo mtuhumiwa huyo akachomoa sime aliyokuwa nayo na kumkata kijana huyo.
Afisa mtendaji wa kata ya Galapo Dorrice Abdala akizungumza na mwandishi wa habari hizi  amekilaani kitendo hicho huku  akieleza kuwa hatua aliyoichukua alitoa taarifa kituo cha polisi cha Gallapo.

Tukio lililotokea ni baya na ni kinyume na haki za binadamu.
Ameongeza kuwa baada ya mtu huyo kufanya tukio hilo alikimbilia kusikojulikana
Naye diwani wa kata ya Galapo  Prosper Fabian Themu alifika katika eneo la tukio na kuwaasa wakazi wa kata yake kusheherekea siku za mwisho wa mwaka kwa amani pamoja na  kutii sheria bila shuruti.

Msimu kama huu siku kuu vuru vurugu hizi na magrupu hayapendezi,watu wajaribu muda wote kutafuta amani ili kuepuka matukio kama hayo.
Mmoja wa  mashuhuda Abdul Athuma  amesema kuwa,nimefika asubuhi  hapa nimekuta mtu kakatwa mkono hapa  nasikia ni kijana wa mzee wa Shaa shaa aliefanya uhalifu huo.
Mganga  wa kituo cha afya Galapo amethibitisha kupokelewa kwa mtu huyo huku akieleza kuwa anaendelea vizuri na matibabu .
Ikumbukwe kwamba  jeshi la polisi mkoa wa Manyara kupitia kwa msemaji wake Agustino Senga limesisistiza wananchi kusheherekea  sherehe hizi za mwisho wa mwaka kwa amani na utulivu na kuongeza kuwa limejipanga kukabiliana na aina yeyote ya uvunjifu wa amani.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top