0
Mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe kuwaomba radhi Watanzania na Bunge kwa kudanganya kuwa fedha za maendeleo zilizotolewa katika bajeti ya mwaka 2017/18 ni asilimia 56 ilhali kamati ya bunge imebaini ni asilimia 22 tu.

Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo iliyowasilishwa jana bungeni jijini Dodoma, Kalanga alisema takwimu nyingi za taarifa za hotuba hiyo zinapingana na za Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Alisema waziri huyo ameonesha fedha za miradi ya maendeleo ya maji zimetolewa kwa asilimia 56 ili kulishawishi Bunge lipitishe bajeti hiyo ilihali wilaya nyingi ikiwamo Monduli hazijatengewa bajeti za mradi wowote mwaka huu.

“Waziri anasema ni asilimia 56 wakati kamati inasema 22, tunataka kujua nani ni mkweli? Alihoji Kalanga.

Akiwasilisha bajeti ya Mhandisi Kamwele katika bajeti ya mwaka 2017/18 hadi kufikia Machi mwaka huu wizara ilipokea fedha za maendeleo Sh bilioni 347.5 sawa na asilimia 56.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top