Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole
amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakitampokea yeyote anayetaka kurudi
ndani ya chama hicho bila kufuata utaratibu.
Kauli
hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni(CUF),
Maulid Said Abdallah Mtulia kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote za
uongozi alizokuwa akizishikilia kwenda CCM.
Polepole aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa CCM mkoa wa Mara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama.
“Ameamua
kule aliko haoni itikadi,haoni siasa, haoni mwelekeo, Chama kina baba
wawili huwezi kuwa na nyumba ina baba wawili alafu utasikiliza watoto
watamsikiliza nani, basi amehama,” alisema Polepole.
“Sasa
mimi niko hapa Musoma mimi nitumie fursa hii anayemuunga mkono ni Rais
wetu ambaye ni mwana CCM kwelikweli na ndiye Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi ikimpendeza afuate utaratibu akiona mazuri ya Rais yule asione
vinaelea kwa mazuri yale asione vimeshushwa vimeundwa na wanaounda
mambo mazuri ya Magufuli ni Chama cha Mapinduzi.”
Post a Comment
karibu kwa maoni