0
"Umuhimu wa kufanya Mageuzi Makubwa ya Chama chetu ni kukirudisha Chama hichi katika misingi kilichoanzishwa". NdgMH. Polepole.

"Kukirudisha Chama hichi kuwa Chama Cha Wanachama, nasio tu kuwa Chama Cha Wanachama bali Chama kinachoshughulika na shida za watu wake kwelikweli" Ndg. H.Polepole.

"Uwanachama wa CCM sio Mkumbo Mkumbo ila ni kuwa na imani"Ndg. H.Polepole

"Tunafanya Mageuzi yatakayo tupatia viongozi waaminifu, waadilifu na wanaochukizwa na Rushwa". Ndg. H. Polepole

"Tunataka viongozi wanyenyekevu hatutaki viongozi Mangi Meza" Ndg. H.Polepole

"Tunataka viongozi ukiwasimamisha wapinzani wanatetemeka".
Ndg. H.Polepole

"Nchi hii hatuna upinzani, upinzani upo ndani ya Chama Chetu kwa watu wachache wasiofaa" H.Polepole

"Chagueni Mgombea ambaye anaamini kwamba udini haupaswi kuwa kigezo cha kuchagua mgombea wa Chama Chetu" Ndg. H.Polepole

"Ni mwiko kwa Kiongozi ama Mgombea Kutoa au kupokea rushwa" Ndg. H.Polepole

"Mgombea yeyote atakayethibitika ameshinda kwa rushwa
Atanyang'anywa ushindi wake, atazuiwa kugombea tena kwa muda utakao amuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa" Ndg. H.Polepole

"Ukweli unatabia moja huwa haupendi kupuuzwa" Ndg. H.Polepole

"Ukihisi umeonewa lalamika, toa sababu"
Ndg. H. Polepole

"Sifa kubwa ya mtu mzima anayejitambua ni kuishi kauli yake".Ndg. H.Polepole

"Kuheshimu watu ni kutofanya kinyume na walivyotarajia" Ndg. H.Polepole

Imetolewa na;

Idara ya Itikadi na Uenezi,
3.12.2017
CHAMA CHA MAPINDUZI.(CCM).

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top