Mashindano ya mbio za wazi Mjini Babati [BABATI HALF
MARATHON] katika mbio za kilomita 5 na kilomita 21 yamefanyika leo yakiwakutanisha
watoto,wanawake na wavulana.
Mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 21 ni Elisante
Sule kutoka wilaya ya Mbulu aliekimbia kwa saa 1:08:29,wa pili ambaye ni
Paskali Mombo kutoka wilaya ya Hanang-Katesh amekimbia kwa saa 1:56:54 wakati
Elikarimu Japhet na kutoka mkoani Singida amemaliza mbio kwa saa 1:02:09.
Washiriki wengine na nafasi zao kwenye mabano ni Emanuel
Joseph kutoka Babati[4],Charles Sule -Mbulu[5]
Musa Migire- Babati [6],Shamba Kishinde-Babati[7],Paulo
Godi –Babati [8],Eliasi Emanuel -Arusha[9] na Ginawe Gidafesta-Hanang-Katesh
10.
Mshindi wa kwanza alijichukulia shilimgi taslimu za
kitanzania 50,000,wa pili 30,000 na wa tatu kanyakua shilingi 20,000.
Kwa upande wa wasichana kilomita 21 walikuwa wawili ambapo
Noella Remmy ameshika nafasi ya kwanza baada ya kukimbia kwa saa 1:18:43
akifuatiwa na Paulina Hangali ambaye amekimbia saa 1:36:19.
Nao watoto walioshiriki mbio hizo kilomita 5 na muda wao ni Boay John mshindi namba moja
aliekimbia kwa kukimbia kwa 14:35:07 na
kupewa zawadi ya pesa shilingi 30,000, wa pili ni Remmy Israel muda 15:17:68
kakabidhiwa shilingi 20,000 na wa tatu ni Mathayo Israel muda wake ni 15:40:50 amepewa
shilingi 10,000,Athanasi Sebastian 26:08:66, [4],Rama Juma 16:33:00 [5],Paulo
Wema 16:35:98 [6]na Marcell Emanuel 16:43:12 [7].
Wakati wasichana ni Joyce Petro 17:38:35,[1]Justina Melkiori
17:59:53 [2],Hadija Mohamedi 19:13:22 [3],Christina
John 19:21:81 [4],Paskalina Ema 19:32:38 [5],Mery John 19:43:46 [6],Joyce Joseph
19:55:25 [7],Zanura Mohammedi 20:8:33 [8],Asha Kumba 20:35:80 [9] pamoja na
Anna Martin 20:41:99 namba 10.
Hata hivyo zawadi hizo zilizotolewa ni ndogo mno
ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo mshindi wa kwanza alikuwa akipatiwa hadi
shilingi milioni moja na washiriki wengine kupatiwa zawadi kwa ajili ya kuwapa
motisha ya kuendelea kushiriki msimu mwingine lakini kwa BABATI HALF MARATHON 2017 walioshiriki wote kuanzia namba nne na
kuendelea wameambulia mikono mitupu,waswahili walisema Mikono mitupu hailambwi.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao baadhi ya
wanariadha walioshiriki katika mbio hizo wamesema kuwa wamesononeka sana kuitwa
jukwaani na kupewa mikono mitupu huku MC akitangaza kuwa ni zawadi
mojawapo.Wameongeza kuwa ni vyema wangeandaliwa chochote hata kama ni kidogo wangeridhika.
Mwenyekiti wa BABATI HALF MARATHON Ali Kericho amesema hii
yote imechangiwa na uongozi uliokuwepo ambao walijichagua wenyewe bila kupigiwa
kura hali inayopekea mambo kwenda bila taratibu.
Mwenyekiti huyo amabye ana muda wa wiki mbili tu tangu
achaguliwe anasema ilimuwia vigumu sana hadi kufika hatua ya kukata tamaa
mashindano hayo kufanyika lakini akapambana na kupata msaada kutoka Halmashauri ya mji wa Babati huku wakisaidiwa
na mwenykiti Mohammedi Kibiki na kuongeza kuwa walipofika kuomba sapoti
walielezwa kuwa wamechelewa kwani kwa
wadau mbalimbali yakiwemo makampuni muda wao ulishakwisha na kufunga mahesabu
ya mwaka .
Akizungumza mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Mohammedi
Kibiki amewaasa wazazi kuwahimiza watoto wao kushiriki katika mchezo wa riadha
ili miaka inayokuja Babati iweze kutembea kifua mbele kwa kuwa na wachezaji wengi wa mchezo huo ambao
umetoa ajira kwa vijana wengi.
Baadhi ya wanariadha wakubwa wakizungumza wamesema kuwa
riadha imewafanya kujua nchi nyingi ambazo katika ndoto zao hawakuwahi kufikira
kama wangweza kufika huko lakini kupitia riadha wameweza kufika nchi mbalimbali
duniani na kupata fedha za kuendesha maisha yao.
Katibu mkuu wa Babati Half Marathon Ernest Martin alisema Babati
half Marathon yanayofanyika kila tarehe 31.12 kila mwaka yanasimamiwa na chama
cha riadha Babati na yamepewa Baraka zote na chama cha riadha Tanzania RT huku
yakiwa na malengo ya kukuza na kuendeleza vipaji,ajira kwa vijana pamoja na
kufunga na kufungua mwaka.
Post a Comment
karibu kwa maoni