Anaandika Gharib Mzinga.
Wadau wote wa kandanda nchini Tanzania wanaukumbuka mwaka
1980 kama kumbukumbu iliyobaki katika historia ya soka la Tanzania,
mwaka huu ndio rasmi timu ya taifa ya Tanzania ilifuzu kucheza michuano
ya mataifa huru Afrika iliyofanyika Nigeria. Michuano hiyo ya AFCON ina
thamani kubwa na inashika nafasi ya pili kwa mataifa ya Africa ukiacha
kombe la dunia. 1980 taifa stars ilikua chini ya mwalimu Slawomir
Wolk raia wa poland Akishirikiana vema na Joel nkaya Bendera, vichwa
hivi viwili vilishirikiana kwa uwezo wao wakaifikisha taifa stars Afcon
ambayo ni ndoto kubwa kwa mataifa mengi kufika hususan ya Africa
Mashariki, Tanzania ilitolewa hatua ya awali kutokana na kupangwa kundi
gumu zaidi likiwa na Egypt, Nigeria na Ivory coast.
walimu hawa waliweza kudhibiti na kuyaongoza vema majina
makubwa katika Soka la Tanzania, wachezaji kama Jella mtagwa wa yanga,
Leodiger Tenga wa Pan Africa, Amir salim wa coastal Union, Mtemi
ramadhani wa simba, Hussein Ngulungu wa Moro united, peter Tino wa Pan
Africa, Boniface mkwasa wa yanga, Othman Mambosasa wa simba na wengine,
waliunganishwa na kua Tanzania.
Ni miaka takriban 37 sasa, hakuna mwalimu mwengine au
wachezaji wengine walioweza kulipa deni hilo la kuipeleka Tanzania
katika michuano hiyo. Labda kikosi cha 2011 cha Jan Paulsen chini ya
nahodha shadrack Nsajigwa, Kelvin Yondani, Juma nyoso, Adam nditi, John
Bocco, Mrisho Ngassa, Juma kaseja kiliweza kwa namna yake kulipa deni la
Kikosi cha 1974 kilichochukua ubingwa wa chalenji chini ya Sanday
manara, Mohammed Bakari Tall, sembuli na wengine. Deni limebaki kwa
taifa stars hii ya sasa, kwa mwalimu na wachezaji, mujitahidi mulipe
hilo deni, Joel Bendera amefariki usiku wa jumatano ya tar 6 katika
hospitali ya muhimbili dar es salaam. Mwalimu wa sasa anatakiwa alipe
deni la Joel Bendera ili furaha ya watanzania irejee na isibaki simanzi
kwenye mioyo pindi jina la Slawomir Wolk na Joel Bendera likitajwa.
Waenziwe wachezaji wa zamani na kukaa nao ili kufahamu
vingi kutoka kwao, hawa wataweza kutoa mwenendo mzuri wa tabia ya
mchezaji, mbinu mbadala, hamasa na hata radhi zao zitasaidia kizazi
hiki, hivyo kuna haja ya kuthamini mchango wao, la sivyo tutaendelea
kudaiwa ushiriki wao wa Afcon milele. Na hapo Slawomir Wolk, Joel
Bendera, na kikosi chake watabakia kua Mashujaa wa muda wote.#Mungu_ibariki_Tanzania
#Mungu_Mrehemu_Joel_Bendera.
Amiin.
Post a Comment
karibu kwa maoni