0


Naibu waziri mhandisi Josephat Kandege amewataka wakala wa bara bara za vijijni na mijini TARURA kuhakikisha kuwa kazi wanazozifanya zitokane na mipango ya Halmashauri husika.
Amesesma Lengo la kuanzishwa kwa TARURA Sio kama chombo ambacho hakitaguswa  la hasha tunataka ile hali iliyokuwa inatokana na madiwani na wabunge kulalamika kwamba wapatiwe hata vipande vya barabara na kujengewa makalvati ili barabara zao zipandishwe hadhi, ili ile thamani ya pesa ionekane, na hivyo TARURA itafanya kazi sawa na TANROADS au zaidi.
Pia naibu waziri ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa Babati inavutia,inatia matumani  na ni salama kwa makazi hivyo kuwataka wananchi waweke uwekezaji mkubwa kwa kuwa miundo mbinu yake ipo vizuri,hakuna mafuriko kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
 Naye Mbunge wa Babati mjini Pauline Gekul akizungumza na  Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Josephat Kandege ,alisema ilivyopita V.I.T ilisaidia katika kurahisisha mradi huu wa Bara bara.
Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi alisema kuwa Babati ni mahali salama na sahihi kwa kuwekeza na kwamba kilichobaki kwa Halmashauri ni kutekeleza mradi wa bara bara uliobakia wa kilomita 4 kuhakikisha zinajengwa katika hali ya ubora kama sehemu ya kilomita 1.6 ambayo imeshakamilika.
Kwa upande wa meneja wa  Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania [TARURA] mjini Babati Mhandisi Innocent Ambrose alisema wamepokea maelekezo ya Naibu waziri na wapo tayari kuyafanyia kazi.
Alisema :Awali  tulikuwa tunatumia mfumo wa Dromas  yaaani tunafanya Annual Road Inventory kila mwaka,ndipo tunapata bara bara ipi tuipe kipaumbele.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top