Licha ya wanakijiji
wa Endanachan Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara kupatiwa huduma ya maji
iliyokuwa kero kubwa kwao,bado wanalalamikia gharama za uchangiaji huduma hiyo
wanalipia shilingi 25 kwa lita 20 wakisema kuwa ni kubwa.
Licha ya wanakijiji wa Endanachan wilaya ya Babati mko wa
Manyara kufurahia mradi wa maji
wameiomba Halmashauri kupunguza gharama za vocha wanazozitumia kwa ajili
ya kufanya malipo ya bili hizo.
Wakizungumza na WALTER HABARI kijijini hapo baada ya kufika
na naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Joseph Kakunda [Mb]
alipokuwa akikagua miradi ya maji na shule katika Halmashauri ya Babati mjini
na Vijijini wamesema kuwa awali kabla ya kupatiwa mradi huo walikuwa wakitumia
maji ya visimani ambayo hata hivyo hayakuwa safi na salama kwa matumizi ya
binadamu.
Akiwa katika mradi huo wa maji katika kijiji hicho Naibu waziri wa TAMISEMI
George Kakunda ameshangazwa na
wanakijiji hao kulalamikia bei ya uchangiaji maji huku akiwataka kutunza mradi
huo ili uendelee kuwasaidia.
Mhandisi wa maji wilaya
Babati Onesmo Joachim akichanganua
gharama za mradi huo ambao pia umejumuisha na michango ya wanakijiji kwa
kueleza kuwa Water Aid walichangia silingi Milioni mia mbili themanini na sita na mia nne
arobaini na tisa {256,684,449},wanakijiji walichangia shilingi milioni ishiri
na tisa { 29,000,000} inafikisha jumla ya shilingi milioni 285,684,419 hadi
kukamilika kwake.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Babati Hamis Idd
Malinga amesema kuwa mradi huo umekuwa ni wa mfano katika mkoa wa Manyara na
unapatikana katika wilaya ya Babati vijijini pekee hali inayowavutia wengi kuja
kuutembelea na kujifunza teknolojia hiyo
mpya inayomwezesha mtumiaji maji kulipia bili kwa kutumia mitandao ya simu na kupatiwa
kadi maalumu katika kupata huduma.
Naibu waziri wa TAMISEMI GEORGE KAKUNDA akiwa Babati
alitembelea pia mradi wa elimu halmashauri ya mji wa Babati shule ya msingi
Mlangi na kuvutiwa na uzuri wa shule hiyo ya kisasa huku akimtaka mhandisi wa
mji ajifunze kupitia mradi wa kilimo cha umwagiliaji kilichopo shuleni hapo
kilichogharimu shilingi milioni kumi kwamba wao waliwezaji kutumia pesa kidogo
katika kuanzisha mradi mkubwa .
Serikali inaendelea kuwapatia huduma za maji wananchi hasawa
wale wa vijijini kwa kubuni namna mbalimbali ya kuwafikishia huduma hizo.
Post a Comment
karibu kwa maoni