0
Yanga haijataka kufanya makosa kama ambavyo wapinzani wao wa jadi, Simba walifanya juzi katika michuano ya Kombe la FA.
Yanga imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Reha FC kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kwa jina la Kombe la FA, jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waliocheka na nyavu ni kiungo Pius Buswita na mshambuliaji Amissi Tambwe na hivyo kusonga mbele katika hatua ya 32 Bora ya michuano hiyo.
Mchezo huo ulikuwa mzuri kwa Tambwe ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu, kurejea kwake kumuekuwa na neema kwa Wanayanga hasa kutokana na safu yao ya ushambuliaji kuonekana kupunguza makali.
Katika mchezo huo Yanga ilikuwa chini ya Kocha Msaidizi wa Yanga, Nsajigwa Shadrack kutokana na bosi wake, George Lwandamina kutokana na kufiwa na mtoto wa kiume nchini Zambia.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Youth Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Nadir Haroub, Andrew Vincent, Papy Tshishimbi, Yusuph Mhilu, Raphael Daud, Amis Tambwe, Pius Buswita na Emmanuel Martin/Said Mussa dk69.
Reha FC; Idrisa Ramadhan, Brian Khiza, Japhary Athuman, Abdul Hassan, Ambele Daud, Zuberi Makame, RajabuMohamed, Silvanus Sostenes/Mohamed Abdallah dk58, Bazo Sentumbi/Mohammed Hassan dk64, Salum Athuman na Idrisa Omary

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top