0
Rais wa Zanzibar, Ali Mohammed Shein ametoa kiasi cha shilingi milioni 3 pamoja na kiwanja kwa kila mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kutokana na timu hiyo.
Nyota 24 walionufaika na zawadi hizo kutoka kwa Raisi ni , Ahmed Ali “Salula” (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi) , Mohammed Abdulrahman “Wawesha” (JKU). Abdallah Haji “Ninja” (Yanga), Mohd Othman  Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed “Sangula” (Jang’ombe Boys), Adeyum Saleh “Machupa” (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Issa Haidar “Mwalala” (JKU).
Abdulla Kheir “Sebo” (Azam), Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe). Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang’ombe), Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa “Banka” (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman “Pwina” (JKU) na Hamad Mshamata (Chuoni).
Suleiman Kassim “Seleembe” (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons),  Feisal Salum (JKU),  Khamis Mussa “Rais” (Jang’ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) , Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).
Aidha, pia Rais Shein pia amewataka Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kuacha kupeleka masuala ya mpira mahakamani kwani kitendo hicho kinarudisha mpira nyuma na kuitia aibu Zanzibar.
Zanzibar Heroes walipoteza mechi ya fainali ya CECAFA dhidi ya Kenya kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1 - 1

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top