Takriban watu 13 wamefariki baada ya
mashua ya uvuvi kugonga na meli kubwa na kusababisha mashua hiyo
kupinduka nje ya pwani ya Korea Kusini.
Watu wengine wawili
hawajulikani waliko na walinzi wa pwani ya Korea Kusini wanasema kuwa
oporesheni ya kuwatafuta na kuwaokoa inaendelea.Mashua hiyo ya uvuvi ya Seonchang-1 ilikuwa imewabeba abiria 20 na wahudumia wawili wakati ajali hiyo ilitokea.
Picha zilionyesha mashua hiyo ikiwa imepinduka.
Ndege za helikopta na na meli kadhaa zinashiriki katika shughuli za kuitafuta.
Kisa hicho kinatajwa kuwa kibaya ziadi nchini Korea Kusini tangu watu 15 waangamiae baharini eneo la Jeju mwaka 2015.
Kabla ya mwaka huo feri ya abiria ilipinduka ambapo zaidi ya watu 300 walifariki wengi wao watoto wa shule.
Post a Comment
karibu kwa maoni