0
Image may contain: 2 people, people standing, crowd and outdoor

Ilikuwa ni mechi ngumu sana ambayo haikuwa na utabiri kama ilivyozoeleka kwa wengi huwa wana matokeo mapemaa.
Image may contain: 3 people, people playing sports and outdoor

Mchezo wa leo ambao ni fainali ilishuhudiwa timu zote mbili zikikamiana vya kutosha mpaka dakika 90 za kawaida za mchezo kumalizika kukiwa hakuna yeyote aliechungulia lango la mwenzake na kulazimika waamuzi wa mchezo huo kuamua kupata mshindi kwa mikwaju ya Penati ambayo imewawezesha Azam Fc ya Tanzania kupata mabao 4-3 URA na kuchukua kombe hilo kwa mara ya pili Mfululizo baada ya kuchukua pia mwaka uliopita.
Piakatika rekodi Azam FC wanatwaa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya nne  baada ya awali kulibeba pia katika miaka ya 2012, 2013 na 2017 wakiipiku Simba SC ya Dar es Salaam iliyotwaa mara tatu 2008, 2011 na 2015.   
Yanga SC ndiye bingwa wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2007 wakati timu nyingine zilizotwaa taji hilo ni Miembeni mwaka 2009, Mtibwa Sugar mwaka 2010 na KCCA ya Uganda mwaka 2014.
Jumla ya timu 11 zilishiriki michuano ya mwaka huu ambazo ni URA, Jamhuri, Mwenge, Azam na Simba zilizokuwa Kundi A na Zimamoto, Mlandege, Yanga, JKU, Taifa Jan’gombe na Singida United zilizokuwa Kundi B.
 

Magoli hayo kwa njia ya Penalti Azam FC yamefungwa  na Nahodha Himid Mao, Yakubu Mohammed, Enock Atta Agyei na Aggrey Morris wakati Bruce Kangwa alimpelekea mikononi mpira kipa wa URA, Alionzi Nafian na penalti za URA zimefungwa na Charles Ssempa, Shafiq Kagimu na Jimmy Kulaba. 
Wafungaji URA ni Charles Ssempa, Shafiq Kagimu na Jimmy Kulaba.
 
Mchezo huo uliohudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein.
Pongezi nyingi zimwendee mlinda mlango wa Azm Fc  Mghana Razack Abalora aliyecheza penalti mbili za wachezaji wa URA.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top