0

Afisa Msajili Halmashauri ya Mji wa Mbulu Ndg. Amina Farijala akitoa maelekezo ya Usajili kwa wazee wa Kata ya Daudi walifika kituoni hapo Kusajiliwa. Aliwapa kipaumbele kwa kutopanga foleni kutokana na baadhi yao umri wao kuwa zaidi ya miaka 84.
Katika hali isiyo ya kawaida Halmashauri ya Mji wa Mbulu, wananchi wake katika marika yote
wamejitokeza Kusajiliwa; Wazee, Watu wazima na Vijana hata wale ambao wametimiza umri
wa miaka 18 mwaka huu ambapo wamefanikiwa kukamilisha usajili katika kata za Uhuru,
Ayamohe, Ayamami, Imboru, Silaloda. kwa sasa Usajili unaendelea katika kata za Daudi,
Marang, Gidamba, Gehandu na Titiwi. Ndg. Prosper Alfred Marmo mwananchi Kata ya Daudi,
Kijiji cha Moringa Kitongoji cha Magasi ni miongoni mwa Vijana waliofikisha miaka 18 mwanzoni
mwa mwaka 2018 amesema ameona ni vyema akatii agizo la Serikali kwa Kujitokeza Kusajiliwa
ili apatiwe Kitambulisho cha Taifa Kitakachomsaidia kumtambulisha katika taasisi mbalimbali
pindi anapohitaji huduma za Kijamii ikiwemo kumsaidia kupata mikopo ya elimu ya juu kirahisi
pindi utakapofika wakati wa yeye kujiunga na Elimu ya Juu. Marmo amesisitiza:'Nisingependa
mikwame kujiunga na elimu ya juu wakati utakapofika'.
'Sasa nina uhakika kwa mimi mzee wa miaka 85 kuwa na Kitambulisho cha Taifa itakuwa ni
rahisi kwangu Kutambulika na kupatiwa huduma za Afya kirahisi kupitia mpango wa serikali
kutoa huduma za Afya kwa wazee bila tozo' maneno hayo yamesemwa na Mzee Michael John
wa Kitongoji cha Getagu Halmashauri ya Mbulu anaeleza jinsi alivyofarijika kwa serikali
kuwakumbuka hata kundi la wazee kwa kupewa fursa ya Kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.
Siasa Qawa Yambo mkazi wa Kitongoji cha Moringa - Halmashauri ya Mbulu mwenye umri wa
makamo anaeleza kufurahishwa na jinsi NIDA kwa Mashirikiano na Halmashauri ya Mji wa
Mbulu walivyowakumbuka kwa kuwasogezea huduma karibu na makazi yao hivyo kuwa rahisi
kwao kushiriki Usajili kwani hawatembei umbali mrefu hadi kufika katika kituo kinachotoa
huduma hiyo.
Afisa Msajili Halmashauri ya Mji - Mbulu Ndg. Amina Farijala amewaasa wananchi kujitahidi
kujitokeza mapema kwenye vituo Kusajiliwa badala ya kufika kwenye vituo vya Usajili majira ya
Mchana/Alasiri kama inavyofanywa na wakazi wengi. Ndg. Farijala amesema 'ninatambua kama
kipindi hiki ni msimu wa kilimo hivyo wakazi wa mbulu ni vema mkajitahidi kupanga ratiba zenu
kwa uwiano ili kuhakikisha kuwa mnafika kwenye vituo vya Usajili kwa wakati na vilevile
shughuli za kilimo zinaendelea. Aidha katika Usajili wa Vitambulisho vya Taifa - Mbulu mwitiko
wa kundi la wazee limekuwa kubwa, ikifuatiwa na kundi la makamo na vijana hususan kwa
wakazi wa kata ya Daudi jambo linaloonnyesha jinsi kasi ya uelewa wa umuhimu wa kuwa na
Vitambulisho vya Taifa unavyoendelea kukua kwa kasi. 'Leo tunatarajia Kusajili wananchi wa
Kata ya Tlawi yenye vijiji vya Guneneda, Tlawi, Boboa na Jaranjar.

Mzee Nayhan Hhando mwenye miaka 79 mkazi wa Kitongoji cha Ampe akipigwa picha kwa kutumia Mashine za Usajili Vitambulisho vya Taifa - BVR na Afisa Msajili Msaidizi wa NIDA Ndg. Pastori Silo.

Ndg. Prosper Alfred Marmo aliyetimiza miaka 18 mwanzoni mwa mwaka 2018 mkazi wa Halmashauri ya Mbulu koa wa Manyara amejitokeza Kusajiliwa akidai angependa kuendelea na elimu ya juu hapo baadae hivyo vema akawa na Kitambulisho mapema ili kimsaidie katika kupata mikopo ya Elimu ya juu kirahisi pindi muda utakapotimu. Anayemsajili ni Ndg. Beauty Patricia Panga – Afisa Msajili Msaidizi - NIDA.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top