Najua wengi wetu tayari tulishawai kuwa kwenye mahusiano na
wengine tuko kwenye mahusiano kwa sasa basi kwa leo hii inakuhusu ambapo
tunaangalia Hatua zinazoonyesha penzi limepoteza muelekeo na kwenda kuachana.
MAWASILIANO KUWA DUNI
Kama mawasiliano yalikuwa ni mara nyingi kama tano kwa siku (kwa
wale walio mbali.), na ukiona yanaaza kushuka hadi mara mbili hadi mwisho
wa siku mawasiliano kukata kabisa. Na kila mmoja akiulizwa swali kwanini anasema
nilibanwa na kazi basi hii ni hatua mbaya sana na hii huwa na athari sana pale
mmoja wa wapenzi anapokuwa na mpenzi mwingine.
HASIRA
ZA MARA KWA MARA.
Hatua hii mpenzi wako huanza kuchukia kila jambo. Utende mema yeye
kwake ni baya. Utajiongelesha ni kama unamuongezea hasira. Hapa ndipo watu huwa
wanafikia kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake amamsaliti.
KUZUNGUMZA
MANENO YASIYOFAA MUWAPO PAMOJA
Hii ni hatua ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Mpenzi
wako hutamuona mchungu kupita kiasi. ukishaona mke wako mara nyingi yeye na
wenzake, hana muda na wewe basi ujue kuna jambo linaendelea ambolo mwisho wake
ni kutengana.
KUDAI
KUTENGANA KILA MARA
Hii ni hatua ya mwisho kabisa na Hapa mpenzi wako utaona ni balaa
tupu. Yaani hafai hata kidogo. Kama una imani ndogo utatamani uondoke uende
mbali ambako hutamwona tena. Hapa hakuna jinsi na usipofanya kama atakavyo
mpenzi wako unaweza kuishia hata gerezani au kuchukua uamuzi wa kumpiga.
ZINGATIA
Kama bado unampenda unapaswa kwenda kuomba msamaha kwa yule uliyemwacha. Kukataliwa kwa mara ya kwanza ni jambo la kawaida, kwani ile picha itaendelea kumrudia. Jifanye kama usikii, fanya hivi zaidi ya mara tano hadi kumi. Mke wako au mme wako ataanza kukuonea huruma na hatimae kuwa naye pamoja
Post a Comment
karibu kwa maoni