Kijana
mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Mohamedy Msangi (28) mkazi wa
Kilakala Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma
za kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa milioni 15 katika taasisi ya
mfuko wa Rais Kanda ya Morogoro.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa jambo
hilo na kusema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa na askari
walifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo ambapo baada ya kuhojiwa
alikiri kufanya kosa hilo kwa kuomba mkopo katika taasisi hiyo
inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.
Matei
amedai kuwa kijana huyo alipoomba mkopo huo aliorodhesha majina ya
vijana wengine wanne akijifanya kuwa vijana hao wamejiunga kwenye
kikundi hicho kisha kupatiwa mkopo huku hao vijana aliowaorodhesha
wakiwa hawana taarifa yoyote.
Mbali
na hilo Kamanda Matei alitoa rai kwa wananchi wa Morogoro na kuwataka
wananchi kuacha wizi "Tuache huu wizi kwa kutumia vyombo vinavyotoa
mikopo kwani mikopo hii imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa chini
na hilo ndiyo lengo la Serikali kuwaondolea watu umasikini ili waweze
kufungua viwanda vidogo vidogo na kujipatia kipato, lakini wapo watu
wanatumia vibaya vikundi hivi" alisema Matei
Post a Comment
karibu kwa maoni