0


Gari pekee la maji ya kuzimia majanga ya Moto yanapotokea linalohudumia mkoa wa Manyara wenye wilaya tano.
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Manyara katika mwaka 2017 limefanikiwa kukusanya shilingi milioni 68 ikiwa ni tozo zilizolipwa na wananchi kwa ajili ya ukaguzi wa kinga na  tahadhari ya moto.

Hayo yameelezwa na Julishaeli Mfinanga Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara wakati akizungumza na WALTER HABARI kuhusu mafanikio waliyoyapata katika mwaka wa 2017 na mikakati ya mwaka 2018.

Kamanda Mfinanga amesema kuwa katika mwaka huo walifanikiwa kutoa elimu mbalimbali kupitia taasisi mbalimbali ikiwemo mashuleni ambapo walianzisha vilabu kwa wanafunzi ambao ni mabalozi wa jeshi hilo la Zimamoto.

Kwa mwaka jana walipata miito ya ajali za moto 13 ambayo saba kati ya hayo walifanikiwa kufika kwa wakati na kuweza kuokoa lakini walishindwa kuzuia ajali nyingine kutokana na kuchelewa kupata taarifa na umbali.

Ameeleza kuwa mikakati waliyonayo katika mwaka wa 2018 ni kuendelea kutoa elimu zaidi katika jamii namna ya kujikinga na majanga ya moto pamoja na kuwafikia watu wengi zaidi.

Hata hivyo Changamoto kubwa inayoikabili jeshi la Zima moto na Uokoaji mkoa wa Manyara ni kuwa na vifaa duni vinavyopelekea kufanya kazi kwa kiwango kisichoridhisha,kwani katika mkoa wa Manyara kuna gari moja pekee linalohudumia mkoa mzima ambao kijiografia

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top