Waheshimiwa
Watanzania, tumepigiwa simu na Wanahabari kutaka kujua msimamo wa CUF
kuhusu uteuzi uliofanywa na CCM dhidi ya Maulidi Saidi Mtulia kugombea
Jimbo la Kinondoni.
Kwanza
tunapenda Watanzania watambue kua Mtulia si Mwanachama wa CUF na katika
hali hiyo, Cuf hawezi kua na sababu yoyote ya kushangazwa na uteuzi
huo.
Pili
Watanzania wanapaswa kutambua kwamba CCM kama Chama wanayohaki ya
kumsimamisha Mtulia kua ni Mgombea wao japo Uamuzi huo unaweza kua na
mtimanyongo kwa wanaccm na hata wasiokua wanaccm kutokana na tamaduni za
CCM au historia ya Mtulia mwenyewe kwakua kabla hajajiuzulu alishakua
Mbunge.
CUF
– Chama cha Wananchi kinamtazama Mtulia kama CHAMBO KWENYE NDOANO YA
KUVULIA SAMAKI, Mtulia ni kivutio cha Utalii, ili Mbuga ya Wanyama
itembelewe na Watalii wengi lazima pawepo na kivutio.
Uteuzi
wa Mtulia utawavuta wengi kwenye CCM wakiwa na Mategemeo kua na wao
wakifanya kama alichofanya Mtulia basi watateuliwa kua Wagombea kwenye
Majimbo yao ya awali.
Lakini
Chambo kwenye NDOANO ni ngumu kumpata ila anarahisisha kuvuliwa au
kupatikana kwa Samaki wengi. CUF – Chama cha Wananchi kitawashinda
Wagombea wa Vyama vingine wataoshiriki kwenye Uchaguzi huo. Tumeshaanza
maandalizi muda mrefu na tuna Mgombea mzuri, tuna uhakika wa kushinda
kwenye Jimbo hilo la Kinondoni.
Wito
wetu kwa Watanzania wajitokeze Kwa wingi kupiga Kura za kukataa
Matumizi mabaya ya Fedha za Umma yanayofanywa na Maulidi Mtulia kwa
kutuingiza kwenye Uchaguzi usiokua wa lazima na CCM nayo kuridhia
Matumizi hayo kwa kurejesha jina la Mtulia kugombea nafasi ambayo alikua
nayo hapo awali. Haya ni matumizi mabaya yalioridhiwa na CCM kwa
kumrejesha Mtulia kama Mgombea wa Jimbo la Kinondoni kupitia CCM.
Watanzania
bado tunachangamoto nyingi katika sekta mbali mbali kama vile Elimu,
Afya na Miundombinu duni ndani ya Nchi yetu ambapo Fedha hizi za
Uchaguzi zingeweza kuelekezwa huko. Kataaeni Matumizi haya kwa kushiriki
kikamilifu kwenye Marejeo ya Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Mwezi
February
HAKI SAWA KWA WOTE
Abdul Kambaya
Mkurugenzi wa Habari Uenezi CUF
Post a Comment
karibu kwa maoni