0


Image result for MBUNGE GEKULMbunge wa Babati Mjini amesema hakuna Halmashauri yeyote hapa nchini inayofanya vizuri kama Babati katika kutoa mikopo  mikubwa kwa vijana na wakina mama akitoa mifano kuwa mikoa mingine wanatoa shilingi milioni 2 lakini kwa Babati wanatoa mpaka shilingi milioni mia moja na hamsini 150.
Mbunge huyo wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Paulina Gekul ameyazungumza hayo katika mkutano wa wadau wa maendeleo Babati mjini  mkoani Manyara uliofanyika ukumbi wa Halmashauri ijumaa Januari 5 2018.
Gekul amesema kuwa halmashauri ya mji wa Babati imekuwa ikipongezwa na viongozi mbalimbali kwa kupokea mikopo ya asilimia kumi 10% ya vijana na wakina mama na kuitumia vizuri. 
'Licha ya kuongozwa na watoto wa kambo akimaanisha [CHADEMA] lakini tumekuwa ni mfano mzuri'aliongeza Gekul.
‘Hakuna halmashauri inayofanya kazi vizuri kama hii licha ya kuongozwa na mama wa kambo akimaanisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo japo hakutaja huku akimwaga sifa kede kwa watumishi wa Halmashauri pamoja na wataalamu’.
Amesema kuwa kazi yao ni kuwatia moyo watumishi na wataalamu na pale tunapoteleza ‘lazima tunakiri kwamba tuna kazi ya kufanya lakini tunapofanya vizuri,tunaamini  hata nyie wadau mnaona lazima mtushike mkono ili twende mbele.’

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top