Watu 32 hawajulikani waliko baada ya meli ya mafuta na ile ya mizigo kugongana mashariki mwa pwani ya China Jumamosi jioni.
Meli ya mafuta ya Sanchi yenye usajili wa Panama ikibeba tani 136,000 za mafuta kutoka Iran ilishika moto baada ya kugongana.Wizara ya uchukuzi nchini China ilisema kuwa watu ambao hawakulinai wali ni wahudumu wa meli wakiwemo 30 raia wa Iran na wawili kutoka Bangladesh.
Wahudumu 21 wa meli ya mizigo wameokolewa.
Picha iliyochapishwa na kituo cha taifa cha CGTN, ilionyesha moto mkubwa na moshi ukitoka kwenye meli ya mafuta.
Ajali hiyo ilitokea karibu kilomita 296 kutoka pwani ya Shanghai.
Meli nane za China zimetimiwa kwa oparesheni ya uokoaji kwa mujibu wa shirika la Xinhua nchini China.
Korea Kusini nayo imetuma meli ya walinzi wa pwani na helikopta kusaidia katika uokoaji.
Meli ya mizigo ya usaljili wa Hog Kong CF Crystal ilikuwa imebeba tani 64,000 za nafaka kutoka Marekani kwenda mkoa wa Guangdong kusini mwa China.
Post a Comment
karibu kwa maoni