0
Image result for yanga scYANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Zimamoto 1-0 kwenye mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bao pekee la Yanga leo limefungwa na kiungo mshambuliaji wa zamani wa JKU, Emmanuel Martin dakika ya 60 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo Juma Mahadhi.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi zake nne, sasa ikilingana na Singida United ambayo yenyewe iko juu kwa wastani wake mzuri wa mabao.
Yanga SC sasa watakutana na Singida United kesho Saa 2:15 usiku katika mchezo wa kuamua nani kinara wa kundi, mechi itakayotanguliwa na mchezo kati ya Simba SC na URA ya Uganda Saa 10:30 jioni Uwanja wa Amaan pia.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top