Jeshi
la polisi linamshikilia Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi
Mgalla Mashaka kwa tuhuma za kushindwa kukarabati Shule ya Sekondari
Kigoma.
Meneja
huyo alikamatwa akituhumiwa kushindwa kukarabati shule ya sekondari
Kigoma kwa wakati licha ya kupewa zaidi ya shilingi milioni mia nne kati
ya mia tisa tangu mwezi wa nane mwaka jana.
Mhandisi
Mgalla amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Joyce Ndalichako, kufanya ukaguzi katika shule hiyo ambayo imeanza
kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya
ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo, mabweni, maabara na vyumba vya
madarasa haujakamilika
Prof.
Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua
tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea. Kutokana na hali hiyo
serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza
masomo wiki ijayo.
Post a Comment
karibu kwa maoni