Mtoto huyo wa kiume ambaye alikuwa akiishi na mama yake pamoja na mdogo
wake wa kike alikutwa juzi jioni akiwa ananing’inia kwenye kamba.
Tukio hilo lilibainika baada ya mdogo wake huyo mwenye umri wa miaka
sita kurejea nyumbani na kukuta mlango ukiwa umefungwa kwa ndani na
jitihada zake za kujaribu kufungua na kuita hazikufanikiwa kwani
hapakuwa na mtu aliyeitikia.
Kutokana na kugonga mlango na kuita kwa muda mrefu, majirani akiwamo
mwenye nyumba walikwenda kumsaidia na walikubaliana kwamba waondoe chuma
kilichokuwa katika mlango ili kumwezesha binti kuingia ndani na kumkuta
kaka yake akiwa ananing’inia kwenye kamba.
Majirani hao walitoa taarifa katika kituo cha Polisi Rongai ambao
walifika na kuchukua mwili wa marehemu na kuuhifadhi katika chumba cha
kuhifadhia maiti cha jiji huku wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Post a Comment
karibu kwa maoni