0


Mwonekano wa jengo kubwa la kisasa la Halmashauri ya mji wa Babati.

Mkutano uliohitishwa leo na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Kibiki Mohamedi Kibiki umeingia dosari baada ya kusitishwa na jeshi la polisi kwa madai ya taarifa za kiintelijensia.
Akizungumza na WALTER HABARI Mh. Kibiki amesema kuwa Mkutano huo uliokuwa umepangwa kufanyika katika stand kuu ya mabasi Babati umezuiliwa na polisi akielezwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Agustine Senga kuwa taarifa zinaonyesha kuwa hautakuwa wa Amani.
Kibiki anasema alipigiwa simu na Mkuu wa upelelezi mkoa wa Manyara ambaye alimhoji kwanini anataka kufanya mkutano bila ya kutoa taarifa,na kujibu kuwa taarifa walishazitoa kwa barua.
Hata hivyo kituo cha mabasi cha mjini Babati ndio kitovu kikuu cha mapato ya Halmashauri ya Babati mjini ambapo ndio makao makuu ya mkoa wa Manyara.
Msemaji wa jeshi la polisi mkoani Manyara Agustine Senga amesema kuwa ni kweli wamezuia mkutano huo kwa sababu haukufuata taratibu zinazohitajika ikiwemo kutoa taarifa siku mbili kabla [saa 48] pamoja na taarifa za kiitelijinsia zilizoonyesha kuwa kungetokea uvunjifu wa amani katika mkutano huo.
WALTER HABARI ilishuhudia magari ya polisi kikosi cha kutuliza ghasia yakiranda mtaani huku yakipita katika eneo la stendi ya mabasi iliyopangwa kufanyika kw mkutano huo.
Kibiki aliongeza kuwa ‘Mimi lengo langu kubwa katika mkutano huo ilikuwa ni kuzungumza na wakazi wa Babati na kutoa taarifa kuhusu mambo mbalimbali ya mji wao’.
Katika tangazo lake mwenyekiti wa Halmashauri iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii pamoja na kutangazwa kupitia gari la matangazo ilisomeka,Nitumie nafasi hii kwa niaba ya kamati ya fedha kuwakaribisha katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kesho tarehe 21.1.2018 [ yaani leo jumapili]saa nane mchana,Kikubwa ni kutoa ufafanuzi/taarifa kuhusu sintofahamu ya Ccm kutaka kukabidhiwa eneo la kituo cha mabasi.
Ikumbukwe kuwa awali ulikuwepo mzozo kati ya Halmashauri na Chama cha Mapinduzi [Ccm] juu ya mmiliki halali wa uwanja wa Kwaraa ambao unatumika na wanafunzi wa shule ya msingi BABATI na Osterbay.Mwenyekiti Kibiki ambaye ni Diwani wa kata ya Babati [CHADEMA] ameeleza kuwa waliunda kamati ya watu tisa yeye akiwa mmoja wao kwenda kwa Waziri pamoja na katibu mkuu ili kupata majibu  ambapo walielezwa kuwa watapatiwa majibu.
 Ameongeza" Mkuu wa mkoa Alexender Mnyeti amemwandikia barua mkurugenzi wa Halmashauri ”Ccm wanataka wakabidhiwe Stand na sisi tunasema haiwezekani”.Alisema Kibiki.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top