0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg.Polepole akiwa kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu wilaya ya Rombo amepokea madiwani watatu wa Chadema Halmashauri ya wilaya ya Rombo,

Juliana Malamsha,(Diwani Viti Maalum), Marta Ushaki ( Diwani Viti Maalum) na Frank Joseph Umega(Kata ya kelamfua Mokala Mamlaka ya Mji Mkuu). 

Wamejiuzulu udiwani wao na nafasi zao zote ndani ya Chadema na wameomba kujiunga na CCM kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya ya Rombo na Kikao cha chama kimewakubalia kujiunga na kuwapokea ndani ya CCM.

Na, Nusu ya Baraza la Madiwani Halmashauri ya Rombo wameomba kujiunga na CCM kwa mujibu wa Ndg.Polepole

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top