Mkumbo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya Usalama kwa mwaka jana.
”Hizi
nguo hazipendezi na si maadili yetu, mnaiga wenzenu wanaovaa kwa
sababu ya hali ya hewa ya kwao sasa tunatangaza kuanza msako mwaka huu
na tutakayemkamata tunamchukua hivyo hivyo hadi mahakamani bila kumpa
nguo ya kujifunika ili ndugu zake wamuone’’. Amesema Mkumbo.
Mkumbo
amefikia uamuzi huo kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ubakaji na
ulawiti tofauti na matukio mengine ambayo yamepungua kutoka na jitihada
za jeshi la polisi.
Ambapo
takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka 2016 matukio ya ubakaji yalikuwa 144
huku mwaka 2017 yameongezeka na kuwa 149, wakati matukio ya ulawiti kwa
mwaka 2016 ni 58 na kuongezeka kwa mwaka 2017 na kuwa 62.
Hata
hivyo amesema kuwa sababu kubwa ya kuongezeka kwa matukio hayo ni
kutokana na mila potofu, imani za waganga wa kienjeji na ukosefu wa
elimu.
Aidha
amewataka watanzania kwa ujumla wafahamu kuwa makosa hayo hayafai na
yana adhabu kubwa ya kifungo cha miaka 30 au cha maisha.
Post a Comment
karibu kwa maoni