0
Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.Maafisa wa Ugiriki wanaoshika doria baharini wamesema wanaizuilia meli iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania ambayo ilikuwa imebeba vilipuzi.
Meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda Libya, kinyume na marufuku iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya.
Maafisa wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi ikiwemo.
"Maafisa wa kushika doria baharini wamezima bomu lililokuwa linasafiri," afisa mkuu wa walinzi hao wa Ugiriki Yiannis Sotiriou aliwaambia wanahabari, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ANA.
Wizara ya Safari za Baharini ilisema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki wikendi baada ya maafisa kupashwa habari na mdokezi.

Ilisindikizwa hadi katika bandari moja kisiwa hicho cha Crete na kufanyiwa ukaguzi.

Sotiriou alisema meli hiyo ambayo ilinaswa Jumamosi ilikuwa pia na kasoro nyingi na haikufaa kuwa baharini.
"Ingesababisha madhara makubwa sana kwa watu na mazingira pia," amenukuliwa na AFP.
Nahodha wa meli hiyo kwa jina Andromeda alidai ilikuwa inasafiri kuelekea Djibouti lakini baadaye ikabainika kwamba ilikuwa inasafiri kuelekea mji wa bandarini wa Misrata nchini Libya.
Shirika la AFP linasema mabaharia hao wanane waliokuwa kwenye meli hiyo watafikishwa mbele ya mwendesha mashtaka leo.
Watano kati ya mabaharia hao ni raia wa India, wawili wa Ukraine na mmoja wa Albania.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top