0

Watu 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiece kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera asubuhi ya leo.
Gari hiyo yenye namba za usajil T.542 DKE ilikuwa ikitokea Wilaya ya Kibondo kuelekea Kahama mkoani Shinyanga, huku maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T.860CGS, T.103 DUJ na T.147 DUJ na yote yapo chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na idadi hiyo ya vifo, na kwamba taarifa zaidi na majina itatolewa baada ya muda mfupi ili kutambua majina ya waliopoteza maisha
Naye Mganga Mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita, na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top