Watu nane wilayani
Kiteto mkoani Manyara wamefariki dunia,huku vyanzo vya vifo hivyo vikidhaniwa
kuwa ni Uyoga sumu na nyama ya Ng’ombe yenye ugonjwa.
Wakati wakazi hao
wakiripotiwa kufariki dunia, zaidi ya ng’ombe 6,000 wilayani humo wamekufa.
Akizungumza na WALTER
HABARI KWA NJIA YA SIMU, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto,Tumaini Magessa amesema mpaka
sasa idara ya mifugo wilayani humo imewasiliana na wataalamu
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambao
wanaendelea na uchunguzi.
Dc.Magessa ameeleza kwamba
wataalamu hao kwa kushirikiana na wengine wa Wizara ya Afya wameshachukua
sampuli kutoka kwa watu waliofariki, ng’ombe waliokufa na Uyoga kwa ajili ya
kufanya uchunguzi.
Aidha amesema Majina ya waliofariki dunia bado hayajapatikana
ila wawili walifariki katika Kata ya Kiperesa, wanne katika Kijiji cha Emat,
Kata ya Magungu na wengine wawili bado hawajajua walikuwa wakazi wa kijiji
kipi.
Hata hivyo Magessa Alisema,
Baada ya ukame, mvua kubwa ilinyesha na majani mapya kuota,ambapo wafugaji wanasema huenda Ng’ombe hao wamekufa kutokana
na kula nyasi hizo ambazo bado hazijakomaa.
Amesema mizoga ya Ng’ombe
waliokufa walikutwa maeneo tofauti, mingine ikiwa barabarani na porini.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka
wananchi wa Kiteto kuendelea kuchukua tahadhari wakati ambapo wanasubiri majibu
ya uchunguzi wa wataalamu.
Post a Comment
karibu kwa maoni