Mawaziri wa Fedha
na Mipango wa Tanzania na Rwanda
wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili
namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka
Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala
hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018.
Katika Mkutano huo
wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia
Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana kupitia
upya taarifa zilizo wasilishwa mezani za pande hizo mbili na kufanya maboresho na pia kuzungumza na
Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Maendeleo
ya Afrika kwa pamoja ili wakati wa kikao kijacho waweze kujadili suala hilo kwa
kuangalia vigezo na masharti ya kupata fedha.
Kikao hicho ambacho
ni cha watalamu kimewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri kutoka Rwanda Mhe. Gatete Claver pamoja na Balozi
wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura na Makatibu wakuu wa wizara hizo na
wajumbe wengine.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James na mwenzake wa Rwanda Bw.
Caleb Rwaungaza, wamesaini maagizo hayo ya Mawaziri kwa ajili ya utekelezaji.
Ikumbukwe kuwa mapema
mwezi huu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Rwanda Paul
Kagame walikubaliana kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Reli kutoka Isaka
Shinyanga hadi Kigali Rwanda na wakatoa maagizo ya kuanza utekelezaji kwa
kuangalia namna ya kupata fedha za mradi huo.
Post a Comment
karibu kwa maoni