Katika kata za Endasak, Wareta,
Dawar, Dirma na Gendabi ambako Usajili unaendeshwa na Ofisi ya Usajili ya
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ya wilayani Hanang` kwa kushirikiana kwa
karibu na ofisi ya Usajili ya wilaya ya Hanang`.
Katika hali isiyo ya
kawaida umati mkubwa wa wakazi wa kata hizo wamejitokeza Kusajiliwa
Vitambulisho vya Taifa jambo ambalo si la kawaida kwani kwa kipindi cha majira
haya wengi huwa kwenye mawindo na kutafuta malisho kwa mifugo yao na baadhi yao
wachache huwa kwenye shughuli za kilimo.
Baadhi ya wananchi wa kata
hizo walipohojiwa kwa nyakati tofauti wameonyesha kuelewa umuhimu na ulazima wa
wao kujitokeza wasajiliwe kwani wameelezwa na watendaji wao wa Kata na
Wenyeviti Serikali za vijiji kuwa kila mkazi mwenye umri wa miaka 18 na zaidi
anatakiwa Kujisajili ili Serikali iweze kutambua wananchi wake wanaoishi wilaya
ya Hanang jambo litakalowasaidia katika utoaji huduma kwa wananchi wake ikiwemo
umiliki wa ardhi bila kubugudhiwa.
Mzee Paskali Gway Pamy wa Kijiji cha
Huwanemba Kata ya Dirma wilayani Hanang` amesema imemlazimu kuachia watoto
mifugo yake ili aweze kukusanya familia yake yote (wenyeumri wa miaka 18 na
zaidi) wakiwemo wake zake ili Wasajiliwe na kupata Kitambulisho cha Taifa.
Naye Afisa Msajili Wilaya
ya Hanang`Ndg. Amwesiga K. Bandio amekiri kuwepo kwa mwitiko mkubwa wa wananchi
katika vituo jambo linalotia moyo.
Inaonyesha kwa sasa wananchi wengi
wamehamasiska sana na kwa sehemu wameshaelewa umuhimu wa kuwa na Kitambulisho
cha Taifa.Ndg. Bandio ameushukuru uongozi wa wilaya kwa kutoa ushirikiano wa
karibu ikiwa ni kutoa maelekezo kwa watendaji kuhakikisha wanaelimisha na kuhamasisha
umma katika Kata, vijiji na vitongoji vyao wajitokeze kusajiliwa kwa wakati.
Aidha ameeleza kwa sasa Ofisi ya Usajili wilaya
anayoisimamia imeshakamilisha Usajili katika kata za Katesh, Ganana, Jorodom,
Dumbeta, Mogitu, Nangwa na Endasak.
![]() | |||||||
Afisa Habari wa NIDA Bi Agnes Gerald akitoa maelekezo kwa mwananchi alipokuwa katika zoezi la Uandikishaji wilaya ya Hanang mkoani Manyara.![]() |
Post a Comment
karibu kwa maoni