
Maafisa wa Iran sasa wanasema kuwa wahudumu wote 32,
wakiwemo raia 30 wa Iran na wawili raia wa Bangladesh wote walifariki.
Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini
maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa.
Meli zingine 13 na kikosi kutoka Iran wamekuwa wakishiriki
katika jitihada za kuokoa licha ya kuwepo hali mbaya ya hewa.
Siku ya Jumamosi wafanyakazi walikuwa wameingia kwenye meli hiyo ambapo
walipata miili ya wahudumu wawili ndani ya mashua ya kuokoa maisha.Waokoaji walipata kisanduku cha kurekodi sarafi lakini wakaondoka haraka kutokana kuwepo moshi na joto jingi.
Post a Comment
karibu kwa maoni